2 Kings 5:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Aramu alikuwa mtu mashuhuri aliyependwa sana na bwana wake, kwani kwa njia yake Mwenyezi-Mungu aliiletea nchi ya Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Mwenyezi Mungu alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ukoma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake Bwana alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Aramu alikuwa mtu mashuhuri aliyependwa sana na bwana wake, kwani kwa njia yake Mwenyezi-Mungu aliiletea nchi ya Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kwa kupitia yeye, BWANA alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, bwana alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Aramu alikuwa mtu mashuhuri aliyependwa sana na bwana wake, kwani kwa njia yake Mwenyezi-Mungu aliiletea nchi ya Aramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Namani, mkuu wa vita wa mfalme wa Ushami, alikuwa mtu mkubwa machoni pa bwana wake na mtu mwenye macheo, kwani Bwana alimtumia, awapatie Washami wokovu. Huyu mtu aliyekuwa fundi wa vita mwenye nguvu akaugua ukoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake, na mwenye kuheshimiwa, kwa sababu kwa mkono wake BWANA alikuwa amewapa Washami kushinda; tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Namani, jemadari wa waaskari wa mufalme wa Aramu, alikuwa mutu mukubwa aliyeheshimiwa sana na bwana wake, maana kwa njia yake Yawe aliiletea inchi ya Waaramu ushindi. Alikuwa askari hodari, lakini alikuwa na ugonjwa wa ukoma.