2 Kings 5:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Naamani alikasirika sana, akaenda zake akisema, “Nilidhani kwamba hakika atanijia na kumwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, apitishe mikono yake juu ya mahali ninapougua na kuniponya!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kupitisha mkono wake juu ya mahali penye ugonjwa ili aniponye ukoma wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la Bwana, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Naamani alikasirika sana, akaenda zake akisema, “Nilidhani kwamba hakika atanijia na kumwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, apitishe mikono yake juu ya mahali ninapougua na kuniponya!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika na kusema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje asimame na kuliitia jina la BWANA Mungu wake na kuweka mkono wake juu ya mahali pagonjwa aniponye ukoma wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la bwana Mwenyezi Mungu wake, na kuweka mkono wake juu ya mahali pagonjwa, aniponye ukoma wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nilidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la BWANA, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Naamani alikasirika sana, akaenda zake akisema, “Nilidhani kwamba hakika atanijia na kumwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wake, apitishe mikono yake juu ya mahali ninapougua na kuniponya!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Namani alipojiendea na kukasirika, akasema: Nimewaza moyoni kwamba: Atanitokea, asimame na kulitambikia Jina la Bwana Mungu wake, kisha pagonjwa apabandikie mkono wake, auponye ukoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Naamani akakasirika, akaondoka, akasema, Tazama, nalidhania, Bila shaka atatoka kwangu, na kusimama, na kuomba kwa jina la BWANA, Mungu wake, na kupitisha mkono wake mahali penye ugonjwa, na kuniponya mimi mwenye ukoma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Namani alikasirika sana, akaenda zake akisema: “Nilizani kwamba hakika atanifikia na kumwomba Yawe, Mungu wake, apitishe mikono yake juu ya pahali ninapogonjwa na kuniponyesha!