2 Kings 5:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo akarudi kwa mtu wa Mungu pamoja na watu wake, akasema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu yeyote ila tu Mungu wa Israeli; kwa hiyo, tafadhali sasa upokee zawadi za mtumishi wako.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo akarudi kwa mtu wa Mungu pamoja na watu wake, akasema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu yeyote ila tu Mungu wa Israeli; kwa hiyo, tafadhali sasa upokee zawadi za mtumishi wako.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na wote aliofuatana nao. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani kote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee zawadi kutoka mtumwa wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo akarudi kwa mtu wa Mungu pamoja na watu wake, akasema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu yeyote ila tu Mungu wa Israeli; kwa hiyo, tafadhali sasa upokee zawadi za mtumishi wako.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akarudi kwa yule mtu wa Mungu, yeye nao wote, aliosafiri nao, akaja, akasimama mbele yake, akasema: Nitazame! Ninajua, ya kuwa hakuna Mungu katika nchi zote, isipokuwa katika nchi ya Isiraeli. Sasa pokea matunzo mkononi mwa mtumishi wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu akarudi kwa mutu wa Mungu pamoja na watu wake, akasema: “Sasa ninajua kwamba hakuna Mungu yeyote katika dunia lakini tu Mungu wa Israeli; kwa hiyo, tafazali sasa upokee zawadi ya mutumishi wako.”