2 Kings 5:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.” Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nabii akajibu, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo, ninayemtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.” Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nabii akajibu, “Hakika kama BWANA aishivyo, ambaye ninamtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nabii akajibu, “Hakika kama bwana aishivyo, ambaye ninamtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elisha akajibu, “Naapa kwa Mwenyezi-Mungu aliye hai ambaye ninamtumikia, kwamba sitapokea zawadi yoyote.” Naamani akamsihi, lakini Elisha akakataa kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajibu: Hivyo, Bwana, ninayemtumikia, alivyo Mwenye uzima, sitachukua cho chote. Akamhimiza, ayachukue, lakini akakataa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini akasema, Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elisha akamujibu: “Kama vile Yawe, yule ambaye mimi ninamutumikia, anavyoishi, sitapokea zawadi yoyote.” Namani akamusihi, lakini Elisha akakataa kabisa.