2 Kings 5:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mwenyezi-Mungu na anisamehe ninapofuatana na mfalme wangu kwenda kuabudu katika hekalu la Rimoni mungu wa Aramu. Naomba Mwenyezi-Mungu anisamehe!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Mwenyezi Mungu na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, Mwenyezi Mungu na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jambo hili Bwana amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, Bwana amwachilie mtumwa wako jambo hili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mwenyezi-Mungu na anisamehe ninapofuatana na mfalme wangu kwenda kuabudu katika hekalu la Rimoni mungu wa Aramu. Naomba Mwenyezi-Mungu anisamehe!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini BWANA na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Wakati bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, BWANA na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini bwana na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Wakati bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, bwana na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jambo hili BWANA amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, BWANA amwachilie mtumwa wako jambo hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mwenyezi-Mungu na anisamehe ninapofuatana na mfalme wangu kwenda kuabudu katika hekalu la Rimoni mungu wa Aramu. Naomba Mwenyezi-Mungu anisamehe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Neno hili tu Bwana na amwondolee mtumishi wako, bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni kutambika mle, naye akijiegemeza mkononi pangu, akijiangusha chini mle nyumbani mwa Rimoni, nami nikijiangusha chini mle nyumbani mwa Rimoni. Basi, neno hili Bwana na amwondolee mtumishi wako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jambo hili BWANA amwachilie mtumwa wako; bwana wangu akiingia nyumbani mwa Rimoni ili aabudu humo, naye akitegemea mkononi mwangu, nami nikijiinama nyumbani mwa Rimoni, hapo ninapojiinama nyumbani mwa Rimoni, BWANA amwachilie mtumwa wako jambo hili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yawe anisamehe ninapofuatana na mufalme wangu kwenda kuabudu katika hekalu la Rimoni mungu wa Waaramu. Ninapaswa kuinama pamoja naye kwa sababu anaegemea kwenye mukono wangu. Ninaomba Yawe anisamehe!”