2 Kings 5:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo akaondoka kumfuata Naamani. Naamani alipotazama na kuona mtu anamfuata mbio, akashuka garini mwake akaenda kukutana naye. Basi, akamwuliza, “Je, kuna usalama?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka gari lake la vita na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo akaondoka kumfuata Naamani. Naamani alipotazama na kuona mtu anamfuata mbio, akashuka garini mwake akaenda kukutana naye. Basi, akamwuliza, “Je, kuna usalama?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka kwenye gari lake na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka kwenye gari lake na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo akaondoka kumfuata Naamani. Naamani alipotazama na kuona mtu anamfuata mbio, akashuka garini mwake akaenda kukutana naye. Basi, akamwuliza, “Je, kuna usalama?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Gehazi akakimbia akimfuata Namani. Namani alipomwona, akimfuata mbiombio, Namani akaruka kutoka garini, akamwendea, akamwuliza: Ni habari njema?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naamani, alipoona mtu apigaye mbio anakuja nyuma yake, alishuka garini amlaki, akasema, Je! Ni amani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hapo akaondoka na kumufuata Namani. Namani alipoangalia na kuona mutu anamufuata mbio, akashuka ndani ya gari lake, akaenda kukutana naye. Basi, akamwuliza: “Kuna usalama?”