2 Kings 5:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa ila tu bwana wangu amenituma nikuambie kwamba sasa hivi amepokea watu wawili wa kundi la manabii katika nchi ya milima ya Efraimu, naye angependa uwape vipande 3,000 vya fedha na mavazi mawili ya sikukuu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha na mavazi mawili.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa ila tu bwana wangu amenituma nikuambie kwamba sasa hivi amepokea watu wawili wa kundi la manabii katika nchi ya milima ya Efraimu, naye angependa uwape vipande 3,000 vya fedha na mavazi mawili ya sikukuu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya kilima cha Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha na mivao miwili ya mavazi.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha na mivao miwili ya mavazi.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana wa manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa ila tu bwana wangu amenituma nikuambie kwamba sasa hivi amepokea watu wawili wa kundi la manabii katika nchi ya milima ya Efraimu, naye angependa uwape vipande 3,000 vya fedha na mavazi mawili ya sikukuu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akasema: Ni njema; bwana wangu amenituma kwamba: Tazama, sasa hivi wamekuja kwangu vijana wawili waliotoka milimani kwa Efuraimu kwa wanafunzi wa wafumbuaji. Wape kipande cha fedha, ndio shilingi 12000 na nguo mbili za sikukuu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, Amani. Bwana wangu amenituma, kusema, Tazama, sasa hivi wamenijia kutoka milimani mwa Efraimu vijana wawili wa wana na manabii; uwape, nakuomba, talanta ya fedha, na mavazi mawili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gehazi akajibu: “Mambo yote ni sawa lakini tu bwana wangu amenituma nikuambie kwamba sasa hivi amepokea watu wawili wa kundi la manabii katika inchi ya milima ya Efuraimu, naye angependa uwape vikoroti elfu tatu vya feza na nguo mbili ya sikukuu.”