2 Kings 5:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naamani akasema, “Tafadhali chukua vipande 6,000 vya fedha.” Akamsihi, kisha akamfungia mafungu mawili na kumpa mavazi mawili ya sikukuu, akawapa watumishi wake wawili na kuwaagiza wafuatane na Gehazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mavazi mawili. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naamani akasema, “Tafadhali chukua vipande 6,000 vya fedha.” Akamsihi, kisha akamfungia mafungu mawili na kumpa mavazi mawili ya sikukuu, akawapa watumishi wake wawili na kuwaagiza wafuatane na Gehazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mivao miwili ya mavazi. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mivao miwili ya mavazi. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamsihi, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakatangulia mbele yake wakiwa wameyabeba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naamani akasema, “Tafadhali chukua vipande 6,000 vya fedha.” Akamsihi, kisha akamfungia mafungu mawili na kumpa mavazi mawili ya sikukuu, akawapa watumishi wake wawili na kuwaagiza wafuatane na Gehazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namani akamwambia: Itafaa, uchukue vipande viwili vya fedha, ndio shilingi 24000; akamhimiza sana, akazifunga zile fedha katika mifuko miwili pamoja na nguo mbili za sikukuu, akampa nao vijana wawili, wamchukulie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naamani akasema, Uwe radhi, ukatwae talanta mbili. Akamshurutisha, akafunga talanta mbili za fedha ndani ya mifuko miwili, na mavazi mawili, akawatwika watumishi wake wawili; nao wakayachukua mbele yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Namani akasema: “Tafazali twaa vikoroti elfu sita vya feza.” Akamusihi, kisha akamufungia mafungu mawili na kumupa nguo mbili ya sikukuu, akawapa watumishi wake wawili na kuwaagiza wafuatane na Gehazi.