2 Kings 5:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipofika mlimani alipoishi Elisha, Gehazi akachukua mafungu ya fedha kutoka kwa watumishi wa Naamani na kuyapeleka ndani, nyumbani mwake. Kisha akawaruhusu wale watumishi waende zao, nao wakaondoka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipofika mlimani alipoishi Elisha, Gehazi akachukua mafungu ya fedha kutoka kwa watumishi wa Naamani na kuyapeleka ndani, nyumbani mwake. Kisha akawaruhusu wale watumishi waende zao, nao wakaondoka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha mbali ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipofika kilimani, alivichukua kutoka mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipofika mlimani alipoishi Elisha, Gehazi akachukua mafungu ya fedha kutoka kwa watumishi wa Naamani na kuyapeleka ndani, nyumbani mwake. Kisha akawaruhusu wale watumishi waende zao, nao wakaondoka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika kilimani akazichukua mikononi mwao, akaziweka mle nyumbani; nao wale watu akawapa ruhusa, wakaenda zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipofika kilimani, alivitwaa mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika juu ya mulima pahali Elisha alipoishi, Gehazi akatwaa mafungu ya feza kutoka kwa watumishi wa Namani na kuyapeleka ndani ya nyumba yake. Kisha akawaruhusu wale watumishi waende zao, nao wakaondoka.