2 Kings 6:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja wao akajibu, “Hakuna anayetusaliti, ee mfalme. Anayehusika ni Elisha, nabii aliyeko huko Israeli. Yeye humwambia mfalme wa Israeli chochote unachosema hata ukiwa katika chumba chako cha kulala.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wa maafisa wake akasema, “Mfalme bwana wangu, hakuna hata mmoja wetu. Lakini Al-Yasa, yule nabii aliye Israeli, humwambia mfalme wa Israeli hata yale maneno unayozungumza katika chumba chako cha kulala.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja wao akajibu, “Hakuna anayetusaliti, ee mfalme. Anayehusika ni Elisha, nabii aliyeko huko Israeli. Yeye humwambia mfalme wa Israeli chochote unachosema hata ukiwa katika chumba chako cha kulala.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wa maafisa wake akasema, “Mfalme bwana wangu, hakuna hata mmoja wetu; lakini Elisha, yule ambaye ni nabii katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli hata yale maneno unayozungumza ukiwa katika chumba chako cha kulala.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wa maafisa wake akasema, “Mfalme bwana wangu, hakuna hata mmoja wetu. Lakini Al-Yasa, yule nabii aliye Israeli, humwambia mfalme wa Israeli hata yale maneno unayozungumza katika chumba chako cha kulala.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja wao akajibu, “Hakuna anayetusaliti, ee mfalme. Anayehusika ni Elisha, nabii aliyeko huko Israeli. Yeye humwambia mfalme wa Israeli chochote unachosema hata ukiwa katika chumba chako cha kulala.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja wao watumishi wake akasema: Sivyo, bwana wangu mfalme, kwani mfumbuaji Elisa alioko kwao Waisiraeli humsimulia mfalme wa Waisiraeli nayo maneno, unayoyasema chumbani mwako mwa kulalia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumoja wao akajibu: “Hakuna anayekuwa upande wake, ee mufalme. Anayefanya vile ni Elisha, nabii anayekuwa kule Israeli. Yeye anamwambia mufalme wa Israeli mambo yote unayosema hata ukiwa katika chumba chako cha kulala.”