2 Kings 6:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Elisha akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika mlima wote, kumzunguka Elisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Al-Yasa akaomba, “Ee Mwenyezi Mungu, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo Mwenyezi Mungu akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya vita yaliyowaka moto yamemzunguka Al-Yasa pande zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Elisha akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika mlima wote, kumzunguka Elisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Elisha akaomba, “Ee BWANA, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo BWANA akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto yote yamemzunguka Elisha pote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Al-Yasa akaomba, “Ee bwana, mfumbue macho huyu mtumishi ili apate kuona.” Ndipo bwana akayafumbua macho ya yule mtumishi, naye akatazama na kuona vilima vimejaa farasi na magari ya moto, yamemzunguka Al-Yasa pande zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Elisha akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika mlima wote, kumzunguka Elisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Elisa akaomba na kusema: Bwana, mfumbue macho, apate kuona! Ndipo, Bwana alipomfumbua yule kijana macho, apate kuona, akaona, ya kuwa huo mlima wote umejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisa pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Elisha akaomba: “Ee Yawe, umufumbue macho kusudi apate kuona!” Basi, Yawe akamufumbua macho yule kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila pahali katika mulima wote, kumuzunguka Elisha.