2 Kings 6:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Adui waliposhuka kumwelekea, Al-Yasa akamwomba Mwenyezi Mungu: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Al-Yasa alivyoomba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipomtelemkia Elisha akamwomba Bwana, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati adui waliposhuka kumwelekea Elisha, Elisha akamwomba BWANA akasema: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Elisha alivyoomba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati adui waliposhuka kumwelekea, Al-Yasa akamwomba bwana: “Wapige watu hawa kwa upofu.” Basi Mungu akawapiga kwa upofu, kama Al-Yasa alivyoomba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipomteremkia Elisha akamwomba BWANA, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale askari walipomshukia, Elisa akamwomba Bwana kwamba: Wapige wamizimu hawa, wapofuke! Akawapiga, wakapofuka, kama Elisa alivyoomba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipomtelemkia Elisha akamwomba BWANA, akasema, Uwapige, nakusihi, watu hawa kwa upofu. Akawapiga kwa upofu sawasawa na neno la Elisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Yawe akisema: “Ninakuomba ufanye watu hawa wakuwe vipofu!” Yawe akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.