2 Kings 6:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asipokusaidia, mimi nitakupa msaada kutoka wapi; kutoka katika kiwanja cha kupuria au kutoka katika shinikizo?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akajibu, “Ikiwa Mwenyezi Mungu hakusaidii, nitakutolea wapi msaada? Je, ni kwenye sakafu ya kupuria? Au ni kwenye shinikizo la kukamulia zabibu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasema, Bwana asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asipokusaidia, mimi nitakupa msaada kutoka wapi; kutoka katika kiwanja cha kupuria au kutoka katika shinikizo?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akajibu, “Ikiwa BWANA hakusaidii, nitapata wapi msaada kwa ajili yako? Je, ni kutoka kwenye sakafu ya kupuria? Au kwenye shinikizo la divai?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akajibu, “Ikiwa bwana hakusaidii, nitakutolea wapi msaada? Je, ni kutoka kwenye sakafu ya kupuria? Au kwenye shinikizo la divai?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasema, BWANA asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya uwanjani mwa kupuria, au ya shinikizoni?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akamwambia, “Mwenyezi-Mungu asipokusaidia, mimi nitakupa msaada kutoka wapi; kutoka katika kiwanja cha kupuria au kutoka katika shinikizo?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akajibu: Bwana asipokusaidia, mimi nitawezaje kukusaidia? Je? Ninacho kitokacho penye kupuria ngano au penye kukamulia zabibu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasema, BWANA asipokusaidia, nikusaidieje mimi? Ya sakafuni, au ya shinikizoni?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamwambia: “Yawe asipokusaidia, mimi nitaweza kukupa musaada kutoka wapi? Kutoka katika kiwanja cha kupepetea ngano au kutoka katika kikamulio?