2 Kings 6:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara mfalme aliposikia maneno ya mwanamke huyo alirarua nguo zake kwa huzuni, na watu waliokuwa karibu na ukuta waliona kwamba alikuwa amevaa vazi la gunia ndani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme aliposikia maneno ya yule mwanamke, akararua mavazi yake. Naye alipoendelea kutembea ukutani, watu wakamtazama, na ndani ya mavazi yake alikuwa amevaa gunia mwilini mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara mfalme aliposikia maneno ya mwanamke huyo alirarua nguo zake kwa huzuni, na watu waliokuwa karibu na ukuta waliona kwamba alikuwa amevaa vazi la gunia ndani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mfalme aliposikia maneno ya yule mwanamke, alirarua majoho yake. Naye Alipoendelea kutembea ukutani, watu wakamtazama, ndani ya majoho yake alikuwa amevaa nguo ya gunia mwilini mwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mfalme aliposikia maneno ya yule mwanamke, alirarua mavazi yake. Naye alipoendelea kutembea ukutani, watu wakamtazama, na ndani ya mavazi yake alikuwa amevaa nguo ya gunia mwilini mwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara mfalme aliposikia maneno ya mwanamke huyo alirarua nguo zake kwa huzuni, na watu waliokuwa karibu na ukuta waliona kwamba alikuwa amevaa vazi la gunia ndani yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme alipoyasikia maneno ya huyu mwanamke, akayararua mavazi yake papo hapo, alipokuwa anatembea bomani; nao watu walipomtazama, wakaona, ya kuwa amevaa gunia ndani penye mwili wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, mfalme alipoyasikia maneno ya huyo mwanamke, aliyararua mavazi yake; (naye alikuwa akipita juu ya ukuta;) na watu wakaona, na tazama, alikuwa amevaa magunia ndani mwilini mwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara mufalme aliposikia maneno ya mwanamuke yule alipasua nguo zake kwa huzuni, na watu waliokuwa karibu na ukuta waliona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia ndani yake.