2 Kings 7:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elisha akamjibu, “Sikiliza neno la Mwenyezi-Mungu: Kesho wakati kama huu, humu Samaria kilo tatu za unga bora wa ngano zitagharimu fedha shekeli moja ya fedha, na kilo sita za shayiri kadhalika zitagharimu fedha shekeli moja.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Al-Yasa akasema, “Sikiliza neno la Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elisha akamjibu, “Sikiliza neno la Mwenyezi-Mungu: Kesho wakati kama huu, humu Samaria kilo tatu za unga bora wa ngano zitagharimu fedha shekeli moja ya fedha, na kilo sita za shayiri kadhalika zitagharimu fedha shekeli moja.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Elisha akasema, “Sikiliza neno la BWANA. Hivi ndivyo asemavyo BWANA: Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Al-Yasa akasema, “Sikiliza neno la bwana. Hivi ndivyo asemavyo bwana: Wakati kama huu kesho, kipimo kimoja cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli moja ya fedha, na vibaba viwili vya shayiri kwa shekeli moja ya fedha katika lango la Samaria.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elisha akasema, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elisha akamjibu, “Sikiliza neno la Mwenyezi-Mungu: Kesho wakati kama huu, humu Samaria kilo tatu za unga bora wa ngano zitagharimu fedha shekeli moja ya fedha, na kilo sita za shayiri kadhalika zitagharimu fedha shekeli moja.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elisa akasema: Sikilizeni neno la Bwana! Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kesho saa zizi hizi pishi ya unga wa ngano itauzwa kwa shilingi mbili na pishi mbili za mawele kwa shilingi mbili hapo mlangoni pa mji huu wa samaria.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elisha akasema, Lisikieni neno la BWANA; BWANA asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elisha akamujibu: “Sikiliza neno la Yawe: Kesho kwa wakati kama huu, humu Samaria kilo tatu za unga bora wa ngano zitanunuliwa kwa kipande kimoja cha feza, na kilo sita za shayiri kwa kipande kimoja cha feza.”