2 Kings 7:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, wakaondoka katika kambi ya Waaramu na kuwaita mabawabu wa mji na kuwaambia: “Tulikwenda katika kambi ya Waaramu na hatukuweza kumwona wala kumsikia mtu yeyote. Farasi na punda wangali wamefungwa, na mahema yako kama walivyoyaacha.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo wakaenda mjini na kuwaita walinzi wa langoni, wakawaambia, “Tulienda katika kambi ya Waaramu lakini hapakuwa na mtu huko, hata sauti ya mtu yeyote, ila farasi na punda waliofungwa, na mahema yaliyoachwa kama yalivyokuwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, wakaondoka katika kambi ya Waaramu na kuwaita mabawabu wa mji na kuwaambia: “Tulikwenda katika kambi ya Waaramu na hatukuweza kumwona wala kumsikia mtu yeyote. Farasi na punda wangali wamefungwa, na mahema yako kama walivyoyaacha.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo wakaenda mjini na kuwaita walinzi wa langoni na kuwaambia, “Tulikwenda katika kambi ya Waaramu wala hapakuwepo na mtu huko, hapakuwa na sauti ya mtu ye yote, ila farasi na punda waliofungwa na mahema yaliyoachwa kama yalivyokuwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo wakaenda mjini na kuwaita walinzi wa langoni, wakawaambia, “Tulikwenda katika kambi ya Waaramu lakini hapakuwepo na mtu huko, hata sauti ya mtu yeyote, ila farasi na punda waliofungwa na mahema yaliyoachwa kama yalivyokuwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu yeyote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, wakaondoka katika kambi ya Waaramu na kuwaita mabawabu wa mji na kuwaambia: “Tulikwenda katika kambi ya Waaramu na hatukuweza kumwona wala kumsikia mtu yeyote. Farasi na punda wangali wamefungwa, na mahema yako kama walivyoyaacha.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaja, wakamwita mngoja lango la mji, wakawapasha habari kwamba: Tumeingia makambini mwa Washami, lakini hamna mtu wala sauti ya mtu, wamo farasi tu waliofungwa na punda waliofungwa, tena mahema yamo vivyo hivyo, yalivyoachwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo, wakaondoka katika kambi ya Waaramu na kuwaita walinda milango ya muji na kuwaambia: “Tulikwenda katika kambi ya Waaramu na hatukuweza kumwona wala kumusikia mutu yeyote. Farasi na punda wangali wanafungwa, na mahema yako kama walivyoyaacha.”