2 Kings 7:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingawa kulikuwa bado giza, mfalme aliamka na kuwaambia maofisa wake, “Mimi najua mpango wa Waaramu! Wanajua tuna njaa mjini, sasa wameacha kambi yao kwenda kujificha ili tutakapokwenda kutafuta chakula, watukamate sote hai na kuuteka mji.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akaamka usiku na kuwaambia maafisa wake, “Nitawaambia kile Waaramu walichotufanyia. Wanajua kwamba tuna njaa, hivyo wameacha kambi yao ili kujificha mashambani, wakifikiri, ‘Kwa hakika watatoka nje ya mji, nasi tutawakamata wakiwa hai na kuingia ndani ya mji.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingawa kulikuwa bado giza, mfalme aliamka na kuwaambia maofisa wake, “Mimi najua mpango wa Waaramu! Wanajua tuna njaa mjini, sasa wameacha kambi yao kwenda kujificha ili tutakapokwenda kutafuta chakula, watukamate sote hai na kuuteka mji.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akaamka usiku na kuwaambia maafisa wake, “Nitawaambia kile Waaramu walichotufanyia. Wanajua kwamba tuna njaa, hivyo wameacha kambi yao ili kujificha mashambani, wakifikiri, ‘Kwa hakika watatoka nje ya mji, nasi tutawakamata wakiwa hai na kuingia ndani ya mji.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akaamka usiku na kuwaambia maafisa wake, “Nitawaambia kile Waaramu walichotufanyia. Wanajua kwamba tuna njaa, hivyo wameacha kambi yao ili kujificha mashambani, wakifikiri, ‘Kwa hakika watatoka nje ya mji, nasi tutawakamata wakiwa hai na kuingia ndani ya mji.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha shambani, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingawa kulikuwa bado giza, mfalme aliamka na kuwaambia maofisa wake, “Mimi najua mpango wa Waaramu! Wanajua tuna njaa mjini, sasa wameacha kambi yao kwenda kujificha ili tutakapokwenda kutafuta chakula, watukamate sote hai na kuuteka mji.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme alipoamka usiku akawaambia watumishi wake: nitawaelezea haya, Washami waliyotufanyizia: Kwa kuwa wanajua, ya kuwa tuko na njaa, wametoka makambini, wajifiche porini kwamba: Watakapotoka mjini, tutawakamata, wakiwa wa hai, kisha tutaingia mjini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akaondoka usiku, akawaambia watumishi wake, Sasa nitawaonyesha ninyi walivyotutendea Washami. Wanajua ya kuwa tuna njaa; basi wametoka kituoni, ili kujificha kondeni, wakisema Watakapotoka mjini, tutawakamata hai; tena tutapata kuingia mjini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ingawa kulikuwa bado giza, mufalme aliamuka na kuwaambia wakubwa wa waaskari wake: “Mimi ninajua mupango wa Waaramu! Wanajua tuna njaa katika muji. Sasa wameacha kambi yao kwenda kujificha kusudi tutakapokwenda kutafuta chakula, watukamate wote tungali wazima na kuuteka muji.”