2 Kings 7:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja kati ya maofisa wake akasema, “Watu wengi tayari wameangamia kama vile wale ambao wamekwisha fariki. Tafadhali utume watu wachache na farasi watano wa wale waliobaki ili waende kuona kumetokea nini.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wa maafisa wake akajibu, “Waamuru watu wachache wakawachukue farasi watano kati ya wale waliobaki katika mji. Hatima yao itakuwa kama ya Waisraeli wote walio hapa. Watakuwa tu kama Waisraeli hawa ambao wanangoja kifo. Hivyo tuwatumeni wajue kumetendeka nini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja kati ya maofisa wake akasema, “Watu wengi tayari wameangamia kama vile wale ambao wamekwisha fariki. Tafadhali utume watu wachache na farasi watano wa wale waliobaki ili waende kuona kumetokea nini.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wa maafisa wake akajibu, “Waamuru watu wachache wakawachukue wale farasi watano waliobaki katika mji. Kama wakipatwa na mambo mabaya huko, haitakuwa hasara kubwa kama vile wangebakia hapa na sisi sote Waisraeli tukafa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wa maafisa wake akajibu, “Waamuru watu wachache wakawachukue farasi watano kati ya wale waliobaki katika mji. Hatima yao itakuwa kama ya Waisraeli wote walio hapa. Watakuwa tu kama Waisraeli hawa ambao wanangoja kifo. Hivyo tuwatumeni wajue kumetendeka nini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kumradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja kati ya maofisa wake akasema, “Watu wengi tayari wameangamia kama vile wale ambao wamekwisha fariki. Tafadhali utume watu wachache na farasi watano wa wale waliobaki ili waende kuona kumetokea nini.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja wao watumishi wake akamjibu akisema: Chukueni farasi watano waliosalia katika wao waliosazwa humu mjini, kwani nao ni sawa kama wale Waisiraeli wengi mno waliosazwa humu mjini, maana nao watakuwa wa kufa tu kama wale Waisiraeli wengi waliokwisha kumalizika. Kwa hiyo na tuwatume, tuone yatakayokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mmojawapo wa watumishi wake akajibu, akasema, Kunradhi; baadhi ya watu na watwae farasi watano katika hao waliosalia, waliobaki ndani ya mji (tazama wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli waliobaki ndani yake; tazama, wamekuwa kama mkutano wote wa Israeli walioangamia), tukawapeleke tukaone.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumoja kati ya wakubwa wake akasema: “Tafazali, utume watu wachache na farasi watano wa wale waliobaki kusudi waende kuona kumetokea nini. Matokeo yao hayatakuwa mabaya zaidi kuliko Waisraeli wote wanaoangamia hapa.”