2 Kings 7:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Samaria wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kama vile Mwenyezi-Mungu alivyosema: Kilo tano za unga safi wa ngano au kilo kumi za shayiri ziliuzwa kwa kipande kimoja cha fedha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kwa hiyo kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Samaria wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kama vile Mwenyezi-Mungu alivyosema: kilo tano za unga safi wa ngano au kilo kumi za shayiri ziliuzwa kwa kipande kimoja cha fedha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kwa hiyo kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli sawasawa kama vile BWANA alivyokuwa amesema.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kwa hiyo kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kama vile bwana alivyokuwa amesema.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Samaria wakatoka na kuteka nyara kambi ya Waaramu. Kama vile Mwenyezi-Mungu alivyosema: Kilo tano za unga safi wa ngano au kilo kumi za shayiri ziliuzwa kwa kipande kimoja cha fedha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, watu wakatoka mjini, wakayateka makambi ya washami. Kisha pishi ya unga wa ngano ikauzwa kwa shilingi mbili na pishi mbili za mawele kwa shilingi mbili, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watu wakatoka, wakaziteka nyara hema za Washami. Ikawa kipimo cha unga mzuri kikauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, sawasawa na neno la BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Samaria wakatoka na kuteka kambi ya Waaramu. Kama vile Yawe alivyosema, kilo tatu za unga bora wa ngano zilinunuliwa kwa kipande kimoja cha feza, na kilo sita za shayiri kwa kipande kimoja cha feza.