2 Kings 7:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye mfalme alikuwa amemweka ofisa mlinzi wake kulinda lango la mji. Ofisa huyo alikanyagwa papo hapo langoni na kuuawa na watu, kama vile Elisha mtu wa Mungu alivyotabiri wakati mfalme alipokwenda kumwona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mfalme alikuwa amemweka yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake awe msimamizi wa lango. Nao watu wakamkanyaga walipoingia langoni, naye akafa, kama vile mtu wa Mungu alivyokuwa ametangulia kusema wakati mfalme alipofika nyumbani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye mfalme alikuwa amemweka ofisa mlinzi wake kulinda lango la mji. Ofisa huyo alikanyagwa papo hapo langoni na kuuawa na watu, kama vile Elisha mtu wa Mungu alivyotabiri wakati mfalme alipokwenda kumwona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mfalme akamweka yule afisa ambaye yeye mfalme alikuwa anautegemea mkono wake awe msimamizi wa lango, nao watu wakamkanyaga walipoingia langoni, naye akafa, kama vile mtu wa Mungu alivyokuwa ametangulia kusema wakati mfalme alipofika nyumbani kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mfalme alikuwa amemweka yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake awe msimamizi wa lango. Nao watu wakamkanyaga walipoingia langoni, naye akafa, kama vile mtu wa Mungu alivyokuwa ametangulia kusema wakati mfalme alipofika nyumbani kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mfalme akamweka yule ofisa mlinzi, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye mfalme alikuwa amemweka ofisa mlinzi wake kulinda lango la mji. Ofisa huyo alikanyagwa papo hapo langoni na kuuawa na watu, kama vile Elisha mtu wa Mungu alivyotabiri wakati mfalme alipokwenda kumwona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yule mkuu wa askari thelathini, ambaye mfalme alimwegemea mkono wake, akamweka langoni mwa mji, awasimamie watu, lakini watu wakamkanyaga mle langoni, akafa palepale, kama yule mtu wa Mungu alivyosema hapo, mfalme aliposhuka kufika kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mfalme akamweka yule akida, ambaye alitegemea mkono wake, awasimamie watu langoni; na watu wakamkanyaga langoni, akafa; kama alivyosema yule mtu wa Mungu, aliyenena hapo mfalme alipomshukia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme alikuwa amemuweka jemadari mulinzi wake kwa kulinda mulango wa muji. Jemadari yule alikanyagwa na watu palepale kwenye mulango, akakufa kama vile Elisha mutu wa Mungu alivyotabiri wakati mufalme alipokwenda kumwona.