2 Kings 7:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kapteni alikuwa amembishia Elisha, akisema, “Kama Mwenyezi-Mungu mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, je, jambo hili lingewezekana?” Naye Elisha alikuwa amemjibu, “Utaona yakitendeka, lakini chakula chenyewe hutakila.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule afisa alikuwa amemwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama Mwenyezi Mungu atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Naye yule mtu wa Mungu alikuwa amemjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na yule akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kapteni alikuwa amembishia Elisha, akisema, “Kama Mwenyezi-Mungu mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, je, jambo hili lingewezekana?” Naye Elisha alikuwa amemjibu, “Utaona yakitendeka, lakini chakula chenyewe hutakila.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule afisa aliyekuwa amemwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama BWANA atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Yule mtu wa Mungu alikuwa amemjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula cho chote kati ya hivyo!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule afisa alikuwa amemwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama bwana atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Naye yule mtu wa Mungu alikuwa amemjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na yule kiongozi akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kapteni alikuwa amembishia Elisha, akisema, “Kama Mwenyezi-Mungu mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, je, jambo hili lingewezekana?” Naye Elisha alikuwa amemjibu, “Utaona yakitendeka, lakini chakula chenyewe hutakila.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, yule mkuu wa askari thelathini alipomjibu yule mtu wa Mungu akisema: Ijapo, Bwana aweke madirisha mbinguni, neno hilo litawezekanaje? Naye yule alikuwa amemjibu: Tazama, na uvione mwenyewe kwa macho yako, lakini hutakula wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na yule akida akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule jemedari mulinzi wa mufalme alikuwa amemwambia Elisha: “Hata kama Yawe mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, jambo hilo litawezekana?” Naye Elisha alikuwa amemujibu: “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hautakula.”