2 Kings 7:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kapteni mwaminifu wa mfalme akamwambia Elisha, “Kama Mwenyezi-Mungu mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, je, jambo hilo litawezekana!” Elisha akamjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake akamwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama Mwenyezi Mungu atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Al-Yasa akajibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kapteni mwaminifu wa mfalme akamwambia Elisha, “Kama Mwenyezi-Mungu mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, je, jambo hilo litawezekana!” Elisha akamjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule afisa ambaye mfalme alikuwa anautegemea mkono wake akamwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama BWANA atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Elisha akajibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula cho chote kati ya hivyo!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule afisa ambaye mfalme alikuwa anauegemea mkono wake akamwambia yule mtu wa Mungu, “Tazama, hata kama bwana atafungua madirisha ya mbinguni, je, jambo hili litawezekana?” Al-Yasa akajibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula chochote kati ya hivyo!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi yule afisa, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kapteni mwaminifu wa mfalme akamwambia Elisha, “Kama Mwenyezi-Mungu mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, je, jambo hilo litawezekana!” Elisha akamjibu, “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hutakula.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mkuu wa askari thelathini, ambaye mfalme alimwegemea mkono wake, alipomjibu yule mtu wa Mungu akisema: Ijapo, Bwana aweke madirisha mbinguni, neno hilo litawezekanaje? Akamjibu: Tazama, na uvione mwenyewe kwa macho yako, lakini hutakula wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Jemedari mulinzi wa mufalme akamwambia Elisha: “Hata kama Yawe mwenyewe angefanya madirisha mbinguni, jambo hilo litawezekana?” Elisha akamujibu: “Utaona kwa macho yako mwenyewe, lakini wewe hautakula.”