2 Kings 7:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakoma wale wanne walipofika pembeni mwa kambi, waliingia ndani ya hema moja, wakala na kunywa vile walivyopata humo, wakachukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuzificha. Wakaingia katika hema nyingine na kufanya vivyo hivyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu wenye ukoma walipofika mwanzoni mwa kambi, wakaingia kwenye mojawapo ya mahema. Wakala na kunywa, na kuchukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuvificha. Wakarudi na kuingia katika hema lingine, na kuchukua baadhi ya vitu kutoka ndani yake na kuvificha pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakoma wale wanne walipofika pembeni mwa kambi, waliingia ndani ya hema moja, wakala na kunywa vile walivyopata humo, wakachukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuzificha. Wakaingia katika hema nyingine na kufanya vivyo hivyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu wenye ukoma walipofika mwanzoni mwa kambi wakaingia kwenye mojawapo ya mahema. Wakala na kunywa, na kuchukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuvificha. Wakarudi na kuingia katika hema jingine, na kuchukua baadhi ya vitu kutoka ndani yake na kuvificha pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu wenye ukoma walipofika mwanzoni mwa kambi, wakaingia kwenye mojawapo ya mahema. Wakala na kunywa, na kuchukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuvificha. Wakarudi na kuingia katika hema jingine, na kuchukua baadhi ya vitu kutoka ndani yake na kuvificha pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakoma wale wanne walipofika pembeni mwa kambi, waliingia ndani ya hema moja, wakala na kunywa vile walivyopata humo, wakachukua fedha, dhahabu na nguo, wakaenda kuzificha. Wakaingia katika hema nyingine na kufanya vivyo hivyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, wale wenye ukoma walipofika pembeni kwa makambi, wakaingia katika hema moja, wakala, wakanywa, wakachukua humo fedha na dhahabu na nguo; kisha wakaenda, wakazichimbia mchangani. Waliporudi wakaingia katika hema jingine, namo humo wakachukua mali, kisha wakaenda kuzichimbia nazo mchangani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale watu wane wenye ukoma walipofika pembeni ya kambi, waliingia ndani ya hema moja, wakakula na kunywa vile walivyopata mule, wakatwaa feza, zahabu na nguo, wakaenda kuzificha. Wakaingia katika hema ingine na kufanya vivyo hivyo.