2 Kings 8:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hazaeli akamwuliza, “Bwana wangu, mbona unalia?” Elisha akamjibu, “Kwa sababu ninajua maovu ambayo utawatendea watu wa Israeli. Utateketeza ngome zao kwa moto, na kuwaua vijana wao, utawapondaponda watoto wao na kuwararua wanawake waja wazito.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hazaeli akauliza “Kwa nini bwana wangu analia?” Al-Yasa akajibu, “Kwa sababu najua mabaya utakayowatendea Waisraeli. Utachoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, kuwatupa chini kwa nguvu watoto wachanga, na kuwatumbua wanawake wenye mimba.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawaseta-seta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hazaeli akamwuliza, “Bwana wangu, mbona unalia?” Elisha akamjibu, “Kwa sababu ninajua maovu ambayo utawatendea watu wa Israeli. Utateketeza ngome zao kwa moto, na kuwaua vijana wao, utawapondaponda watoto wao na kuwararua wanawake waja wazito.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hazaeli akauliza “Kwa nini bwana wangu analia?” Elisha akajibu, “Kwa sababu najua mabaya utakayowatendea Waisraeli. Utachoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, kuwatupa chini kwa nguvu watoto wachanga na kuwatumbua wanawake wenye mimba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hazaeli akauliza “Kwa nini bwana wangu analia?” Al-Yasa akajibu, “Kwa sababu najua mabaya utakayowatendea Waisraeli. Utachoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, kuwatupa chini kwa nguvu watoto wachanga, na kuwatumbua wanawake wenye mimba.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawasetaseta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hazaeli akamwuliza, “Bwana wangu, mbona unalia?” Elisha akamjibu, “Kwa sababu ninajua maovu ambayo utawatendea watu wa Israeli. Utateketeza ngome zao kwa moto, na kuwaua vijana wao, utawapondaponda watoto wao na kuwararua wanawake waja wazito.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hazaeli akamwuliza: Mbona bwana wangu analia machozi? Akajibu: Kwani ninajua, ya kama utawafanyizia wana wa Isiraeli mabaya, miji yao yenye maboma utaiteketeza kwa moto, vijana wao wenye nguvu utawaua kwa panga, wachanga wao utawaponda nao wanawake wao wenye mimba utawatumbua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawaseta-seta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hazaeli akamwuliza: “Bwana wangu, mbona unalia?” Elisha akamujibu: “Kwa sababu ninajua maovu ambayo utawatendea watu wa Israeli. Utateketeza kuta zao kwa moto, na kuwaua vijana wao, utawapondaponda watoto wao na kupasua wanawake wenye mimba tumbo.”