2 Kings 8:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo Yoramu aliondoka na magari yake yote kwenda Zairi. Wakati wa usiku alitoka na makamanda wake wa magari akawashambulia Waedomu waliokuwa wamemzunguka; lakini jeshi lake lilikimbia nyumbani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yehoramu akaenda Sairi pamoja na magari yake yote ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. Hata hivyo, jeshi lake likatorokea nyumbani mwao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na maakida wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo Yoramu aliondoka na magari yake yote kwenda Zairi. Wakati wa usiku alitoka na makamanda wake wa magari akawashambulia Waedomu waliokuwa wamemzunguka; lakini jeshi lake lilikimbia nyumbani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yehoramu akaenda Seiri pamoja na magari yake yote ya vita. Waedomu wakamzunguka pamoja na jemadari wake wa jeshi wa magari ya vita. Lakini akaondoka usiku na kuwashambulia Waedomu waliokuwa wamemzunguka, hata hivyo, jeshi lake likakimbia kurudi nyumbani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yehoramu akaenda Sairi pamoja na magari yake yote ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. Hata hivyo, jeshi lake likatorokea nyumbani mwao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na makamanda wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo Yoramu aliondoka na magari yake yote kwenda Zairi. Wakati wa usiku alitoka na makamanda wake wa magari akawashambulia Waedomu waliokuwa wamemzunguka; lakini jeshi lake lilikimbia nyumbani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yoramu alipoondoka kwenda Sairi akiyachukua magari yote; ikawa, alipoondoka usiku, akawapiga Waedomu waliomzunguka yeye na wakuu wa magari lakini watu walikuwa wameyakimbilia mahema yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na maakida wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Yoramu aliondoka na magari yake yote kwenda Sairi. Wakati wa usiku alitoka na waongozi wake wa magari akawashambulia Waedomu waliokuwa wamemuzunguka. Lakini waaskari wake walikimbilia kwao.