2 Kings 8:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha mfalme Yoramu akarudi mjini Yezreeli ili apate kutibiwa majeraha aliyoyapata huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda alimwendea Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Mfalme Yoramu akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyojeruhiwa na Waaramu huko Ramothi alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli jeraha walizotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa hawezi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha mfalme Yoramu akarudi mjini Yezreeli ili apate kutibiwa majeraha aliyoyapata huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda alimwendea Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Mfalme Yoramu akarudi Yezreeli ili apate kutibu majeraha aliyoyapata huko Ramoth alipokuwa anapigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda, akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Mfalme Yoramu akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyojeruhiwa na Waaramu huko Ramothi alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli majeraha waliyotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha mfalme Yoramu akarudi mjini Yezreeli ili apate kutibiwa majeraha aliyoyapata huko Rama, alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda alimwendea Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa mgonjwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo mfalme Yoramu akarudi Izireeli, apate watakaomponya vidonda, Washami walivyompiga kule Rama, alipopigana na Hazaeli, mfalme wa Ushami. Ndipo, Ahazia, mwana wa Yoramu, mfalme wa Wayuda, aliposhuka kumtazama Yoramu, mwana wa Ahabu, huko Izireeli, kwani ndiko, alikougulia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akarudi Yoramu mfalme, auguzwe katika Yezreeli jeraha walizotia Washami huko Rama alipopigana na Hazaeli mfalme wa Shamu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka amtazame Yoramu mwana wa Ahabu huko Yezreeli, kwa sababu alikuwa hawezi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme Yoramu akarudi katika muji Yezereheli kusudi apate kutunzwa vidonda alivyoumizwa na Waaramu kule Rama, alipopigana na Hazaeli mufalme wa Aramu. Naye Ahazia mwana wa Yehoramu, mufalme wa Yuda alimwendea Yoramu mwana wa Ahabu kule Yezereheli, kwa sababu alikuwa mugonjwa.