2 Kings 8:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Gehazi alipokuwa anamweleza mfalme jinsi Elisha alivyofufua mtu aliyekufa, mwanamke huyo alitoa ombi lake kwa mfalme. Gehazi akasema, “Ee mfalme; huyu ndiye mwanamke ambaye Elisha alimfufua mwanawe!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Gehazi alipokuwa akimweleza mfalme jinsi Al-Yasa alivyomfufua mtu, yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa na Al-Yasa akaja ili amsihi mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, “Huyu ndiye huyo mwanamke, bwana wangu mfalme, na huyu ndiye mwanawe ambaye Al-Yasa alimfufua.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, alipokuwa katika kumwambia mfalme jinsi alivyomfufua mtu aliyekufa, tazama, huyo mwanamke aliyemfufulia mwanawe, alimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, Bwana wangu mfalme, huyu ndiye mwanamke, na huyu ndiye mwanawe, ambaye Elisha alimfufua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Gehazi alipokuwa anamweleza mfalme jinsi Elisha alivyofufua mtu aliyekufa, mwanamke huyo alitoa ombi lake kwa mfalme. Gehazi akasema, “Ee mfalme; huyu ndiye mwanamke ambaye Elisha alimfufua mwanawe!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Gehazi alipokuwa akimweleza mfalme jinsi Elisha alivyomfufua mtu, yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa na Elisha akaja ili amwombe mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, “Huyu ndiye huyo mwanamke, bwana wangu mfalme, na huyu ndiye mwanawe ambaye Elisha alimfufua.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Gehazi alipokuwa akimweleza mfalme jinsi Al-Yasa alivyomfufua mtu, yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa na Al-Yasa akaja ili amsihi mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, “Huyu ndiye huyo mwanamke, bwana wangu mfalme, na huyu ndiye mwanawe ambaye Al-Yasa alimfufua.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, alipokuwa katika kumwambia mfalme jinsi alivyomfufua mtu aliyekufa, tazama, huyo mwanamke aliyemfufulia mwanawe, alimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, Bwana wangu mfalme, huyu ndiye mwanamke, na huyu ndiye mwanawe, ambaye Elisha alimfufua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Gehazi alipokuwa anamweleza mfalme jinsi Elisha alivyofufua mtu aliyekufa, mwanamke huyo alitoa ombi lake kwa mfalme. Gehazi akasema, “Ee mfalme; huyu ndiye mwanamke ambaye Elisha alimfufua mwanawe!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akawa akimsimulia mfalme, jinsi alivyomrudisha yule mfu uzimani, mara yule mwanamke, aliyemfufulia mwanawe, akawako akimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na ya shamba lake. Ndipo, Gehazi alipomwambia: Bwana wangu mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, naye huyu ndiye mwanawe, Elisa aliyemfufua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, alipokuwa katika kumwambia mfalme jinsi alivyomfufua mtu aliyekufa, tazama, huyo mwanamke aliyemfufulia mwanawe, alimlilia mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. Gehazi akasema, Bwana wangu mfalme, huyu ndiye mwanamke, na huyu ndiye mwanawe, ambaye Elisha alimfufua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Gehazi alipokuwa anamwambia mufalme jinsi Elisha alivyofufua mutu aliyekufa, mwanamuke yule alitoa ombi lake kwa mufalme. Gehazi akasema: “Ee mufalme; huyu ndiye mwanamuke ambaye Elisha alimufufua mwana wake!”