2 Kings 8:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hazaeli akapakia zawadi za kila aina ya mazao ya Damasko kiasi cha mizigo ya ngamia arubaini na kumpelekea Elisha. Alipofika kwa Elisha alimwambia, “Mtumishi wako, Ben-hadadi, mfalme wa Aramu amenituma kwako; yeye anauliza, ‘Nitapona ugonjwa huu?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hazaeli akaenda kumlaki Al-Yasa, akiwa amechukua zawadi ya kila kitu kizuri kilichopatikana Dameski, mizigo iliyobebwa na ngamia arobaini. Akaingia ndani na kusimama mbele yake, akasema, “Mwanao Ben-Hadadi mfalme wa Aramu amenituma niulize, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, za kila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mizigo ya ngamia arobaini, akaenda, akasimama mbele yake akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, amenituma kwako, kusema, Je nitapona ugonjwa huu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hazaeli akapakia zawadi za kila aina ya mazao ya Damasko kiasi cha mizigo ya ngamia arubaini na kumpelekea Elisha. Alipofika kwa Elisha alimwambia, “Mtumishi wako, Ben-hadadi, mfalme wa Aramu amenituma kwako; yeye anauliza, ‘Nitapona ugonjwa huu?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hazaeli akaenda kumlaki Elisha, akiwa amechukua kila kitu kizuri kilichopatikana Dameski, mizigo iliyobebwa na ngamia arobaini. Akaingia ndani na kusimama mbele yake, akasema, “Mwanao Ben-Hadadi mfalme wa Aramu amenituma niulize, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hazaeli akaenda kumlaki Al-Yasa, akiwa amechukua zawadi ya kila kitu kizuri kilichopatikana Dameski, mizigo iliyobebwa na ngamia arobaini. Akaingia ndani na kusimama mbele yake, akasema, “Mwanao Ben-Hadadi mfalme wa Aramu amenituma niulize, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, za kila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mizigo ya ngamia arobaini, akaenda, akasimama mbele yake akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, amenituma kwako, kusema, Je nitapona ugonjwa huu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hazaeli akapakia zawadi za kila aina ya mazao ya Damasko kiasi cha mizigo ya ngamia arubaini na kumpelekea Elisha. Alipofika kwa Elisha alimwambia, “Mtumishi wako, Ben-hadadi, mfalme wa Aramu amenituma kwako; yeye anauliza, ‘Nitapona ugonjwa huu?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hazaeli akaenda kuonana naye akichukua mkononi mwake matunzo yote yaliyokuwa vitu vizuri vya Damasko, ya kuchukuliwa na ngamia 40. Alipofika akaja kusimama mbele yake, akamwambia: Mwanao Benihadadi, mfalme wa Ushami, amenituma kwako kukuuliza kwamba: Nitapona ugonjwa huu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi mkononi mwake, za kila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mizigo ya ngamia arobaini, akaenda, akasimama mbele yake akasema, Mwana wako Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, amenituma kwako, kusema, Je nitapona ugonjwa huu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hazaeli akapakia zawadi za kila aina ya mazao ya Damasiki kipimo cha mizigo ya ngamia makumi ine na kumupelekea Elisha. Alipofika kwa Elisha alimwambia: “Mutumishi wako, Beni-Hadadi, mufalme wa Aramu amenituma kwako. Yeye anauliza: ‘Nitapona ugonjwa huu?’ ”