2 Kings 9:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yehu mwana wa Yehoshafati, ambaye pia alikuwa mjukuu wa Nimshi, alikula njama dhidi ya Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoth-gileadi kulinda zamu dhidi ya mfalme Hazaeli wa Aramu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akapanga njama dhidi ya Yoramu. (Wakati huu, Yoramu na Waisraeli wote walikuwa wakiilinda Ramoth-Gileadi dhidi ya Hazaeli mfalme wa Aramu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akafanya fitina juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiulinda Ramoth-Gileadi, yeye na Israeli wote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yehu mwana wa Yehoshafati, ambaye pia alikuwa mjukuu wa Nimshi, alikula njama dhidi ya Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoth-gileadi kulinda zamu dhidi ya mfalme Hazaeli wa Aramu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akafanya shauri baya dhidi ya Yoramu. (Wakati huu, Yoramu na Israeli wote walikuwa wakiilinda Ramoth-Gileadi dhidi ya Hazaeli mfalme wa Aramu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yehu mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akafanya shauri baya dhidi ya Yoramu. (Wakati huu, Yoramu na Israeli wote walikuwa wakiilinda Ramoth-Gileadi dhidi ya Hazaeli mfalme wa Aramu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akamfitinia Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiulinda Ramoth-Gileadi, yeye na Israeli wote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yehu mwana wa Yehoshafati, ambaye pia alikuwa mjukuu wa Nimshi, alikula njama dhidi ya Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoth-gileadi kulinda zamu dhidi ya mfalme Hazaeli wa Aramu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yehu, mwana wa Yosafati, mwana wa Nimusi, akamlia Yoramu njama. Ni hapo, Yoramu alipokuwa akiulinda mji wa Ramoti wa Gileadi, yeye na Waisiraeli wote, usichukuliwe na Hazaeli, mfalme wa Ushami.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo Yehu, mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi, akafanya fitina juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiulinda Ramoth-Gileadi, yeye na Israeli wote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yehu mwana wa Yosafati, ambaye vilevile alikuwa mujukuu wa Nimusi, alifanya mupango wa kuasi Yoramu. Yoramu na watu wote wa Israeli walikuwa Ramoti-Gileadi kwa kulinda zamu juu ya mufalme Hazaeli wa Aramu.