2 Kings 9:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mlinzi aliyekuwa kwa zamu juu ya mnara wa Yezreeli akasema, “Naona watu wakija na gari!” Yoramu akajibu, “Chagua mpandafarasi mmoja, umtume ili akutane nao, awaulize ‘Kuna amani?’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mlinzi aliyesimama juu ya kinara cha Yezreeli alipoona askari wa Yehu wanakuja, akaita akisema, “Naona askari wanakuja.” Yoramu akaamuru, “Mtwae mpanda farasi umtume akakutane nao na kuuliza, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi mlinzi alikuwa anasimama juu ya mnara wa Yezreeli, akaliona lile kundi la watu wa Yehu, alipokuwa akija, akasema, Naona kundi la watu. Yoramu akasema, Haya! Mtwae mpanda farasi mmoja, ukampeleke aende kuwalaki, na kuwauliza, Je! Ni amani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mlinzi aliyekuwa kwa zamu juu ya mnara wa Yezreeli akasema, “Naona watu wakija na gari!” Yoramu akajibu, “Chagua mpandafarasi mmoja, umtume ili akutane nao, awaulize ‘Kuna amani?’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mlinzi asimamaye juu ya kinara cha Yezreeli alipoona askari wa Yehu wanakuja, akaita akisema, “Naona askari wanakuja.” Yoramu akaamuru, “Mtwae mpanda farasi umtume akakutane nao na kuuliza, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mlinzi aliyesimama juu ya kinara cha Yezreeli alipoona askari wa Yehu wanakuja, akaita akisema, “Naona askari wanakuja.” Yoramu akaamuru, “Mtwae mpanda farasi umtume akakutane nao na kuuliza, ‘Je, mmekuja kwa amani?’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi mlinzi alikuwa anasimama juu ya mnara wa Yezreeli, akaliona lile kundi la watu wa Yehu, alipokuwa akija, akasema, Naona kundi la watu. Yoramu akasema, Haya! Mtwae mpanda farasi mmoja, ukampeleke aende kuwalaki, na kuwauliza, Je! Ni amani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mlinzi aliyekuwa kwa zamu juu ya mnara wa Yezreeli akasema, “Naona watu wakija na gari!” Yoramu akajibu, “Chagua mpandafarasi mmoja, umtume ili akutane nao, awaulize ‘Kuna amani?’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mlinzi aliyesimama mnarani juu kule Izireeli alipoliona kundi zima la Yehu, likija, akasema: Mimi naona kundi zima la watu! Ndipo, Yoramu alipomwambia: Chukua mpanda farasi, mtume kuwaendea njiani, awaulize: Mwaleta habari njema?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi mlinzi alikuwa anasimama juu ya mnara wa Yezreeli, akaliona lile kundi la watu wa Yehu, alipokuwa akija, akasema, Naona kundi la watu. Yoramu akasema, Haya! Mtwae mpanda farasi mmoja, ukampeleke aende kuwalaki, na kuwauliza, Je! Ni amani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulinzi aliyekuwa kwenye zamu juu ya munara wa Yezereheli akasema: “Ninaona watu wakikuja na gari!” Yoramu akajibu: “Chagua askari mupanda-farasi mumoja, umutume kusudi akutane nao, awaulize: ‘Munakuja kwa amani?’ ”