2 Kings 9:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yehu akamwambia msaidizi wake Bidkari, “Chukua hiyo maiti yake uitupe katika shamba hilo la Nabothi Myezreeli. Kwa maana, kumbuka wewe na mimi tulipokuwa tumepanda farasi wetu nyuma ya baba yake Ahabu, jinsi Mwenyezi-Mungu alivyonena maneno haya dhidi yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehu akamwambia Bidkari, mwendeshaji wa gari lake la vita, “Mwinue na umtupe katika shamba lililokuwa mali ya Nabothi, Myezreeli. Kumbuka jinsi mimi na wewe tulivyokuwa tukiendesha pamoja magari yetu ya vita nyuma ya Ahabu baba yake, wakati Mwenyezi Mungu alitoa unabii huu kumhusu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Yehu akamwambia Bidkari, akida wake, Mtwae ukamtupe katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli; maana kumbuka, hapo mimi na wewe tulipokuwa tumepanda farasi zetu, na kumfuata Anabu baba yake, Bwana alimwekea mzigo huu, akasema;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yehu akamwambia msaidizi wake Bidkari, “Chukua hiyo maiti yake uitupe katika shamba hilo la Nabothi Myezreeli. Kwa maana, kumbuka wewe na mimi tulipokuwa tumepanda farasi wetu nyuma ya baba yake Ahabu, jinsi Mwenyezi-Mungu alivyonena maneno haya dhidi yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehu akamwambia Bidkari, msaidizi wa gari lake, “Mwinue na umtupe katika shamba lililokuwa mali ya Nabothi, Myezreeli. Kumbuka jinsi mimi na wewe tulivyokuwa tukiendesha pamoja magari yetu nyuma ya Ahabu baba yake wakati BWANA alipotoa unabii huu kumhusu:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehu akamwambia Bidkari, mwendeshaji wa gari lake, “Mwinue na umtupe katika shamba lililokuwa mali ya Nabothi, Myezreeli. Kumbuka jinsi mimi na wewe tulivyokuwa tukiendesha pamoja magari yetu nyuma ya Ahabu baba yake, wakati bwana alipotoa unabii huu kumhusu:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Yehu akamwambia Bidkari, msaidizi wake, Mtwae ukamtupe katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli; maana kumbuka, hapo mimi na wewe tulipokuwa tumepanda farasi zetu, na kumfuata Ahabu baba yake, BWANA alimwekea mzigo huu, akasema;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yehu akamwambia msaidizi wake Bidkari, “Chukua hiyo maiti yake uitupe katika shamba hilo la Nabothi Myezreeli. Kwa maana, kumbuka wewe na mimi tulipokuwa tumepanda farasi wetu nyuma ya baba yake Ahabu, jinsi Mwenyezi-Mungu alivyonena maneno haya dhidi yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akamwagiza Bidekari aliyekuwa mkuu wa askari thelathini: Mchukue, umtupe penye shamba la Naboti wa Izireeli! Kumbuka, mimi na wewe tulipomfuata baba yake Ahabu na kupanda farasi sisi wawili, hapo Bwana alilitoa tamko lile la kumtisha kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Yehu akamwambia Bidkari, akida wake, Mtwae ukamtupe katika kiwanja cha Nabothi, Myezreeli; maana kumbuka, hapo mimi na wewe tulipokuwa tumepanda farasi zetu, na kumfuata Anabu baba yake, BWANA alimwekea mzigo huu, akasema;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yehu akamwambia musaidizi wake Bidikari: “Kamata hiyo maiti yake uitupe katika shamba hilo la Naboti wa Yezereheli. Kwa maana, kumbuka wewe na mimi tulipokuwa tumepanda juu ya farasi wetu nyuma ya baba ya Ahabu, jinsi Yawe alivyosema maneno haya juu yake.