2 Kings 9:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ahazia mfalme wa Yuda alipoona yaliyotukia alikimbia akielekea Nyumba ya Bustani, huku akifuatwa na Yehu. Yehu akawaamuru watu wake, “Muueni naye pia!” Nao wakampiga mshale akiwa garini kwenye njia ya kupanda Guri karibu na mji wa Ibleamu. Halafu alikimbilia Megido na kufia huko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ahazia mfalme wa Yuda alipoona kilichotokea, akakimbia kupitia barabara ya Beth-Hagani. Yehu akamkimbiza akipaza sauti na kusema, “Muue naye pia!” Wakamjeruhi katika gari lake la vita kwenye njia inayoelekea Guri karibu na Ibleamu, lakini akatorokea Megido, akafia huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Ahazia mfalme wa Yuda alipoona hayo, akakimbia kwa njia ya nyumba ya bustanini. Yehu akamfuatia, akasema, Mpigeni huyu naye katika gari lake; wakampiga hapo penye kupandia Guri, karibu na Ibleamu. Akakimbilia Megido, akafa huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ahazia mfalme wa Yuda alipoona yaliyotukia alikimbia akielekea Nyumba ya Bustani, huku akifuatwa na Yehu. Yehu akawaamuru watu wake, “Muueni naye pia!” Nao wakampiga mshale akiwa garini kwenye njia ya kupanda Guri karibu na mji wa Ibleamu. Halafu alikimbilia Megido na kufia huko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Ahazia mfalme wa Yuda alipoona kilichotokea, akakimbia kupitia barabara ya Beth-Hagani. Yehu akamkimbiza akipiga kelele akisema, “Mwue naye pia!” Wakamjeruhi katika gari lake kwenye njia ielekeayo Guri karibu na Ibleamu, lakini akatorokea Megido na akafia huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Ahazia mfalme wa Yuda alipoona kilichotokea, akakimbia kupitia barabara ya Beth-Hagani. Yehu akamkimbiza akipaza sauti na kusema, “Muue naye pia!” Wakamjeruhi katika gari lake kwenye njia ielekeayo Guri karibu na Ibleamu, lakini akatorokea Megido na akafia huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Ahazia mfalme wa Yuda alipoona hayo, akakimbia kwa njia ya nyumba ya bustanini. Yehu akamfuatia, akasema, Mpigeni huyu naye katika gari lake; wakampiga hapo penye kupandia Guri, karibu na Ibleamu. Akakimbilia Megido, akafa huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ahazia mfalme wa Yuda alipoona yaliyotukia alikimbia akielekea Nyumba ya Bustani, huku akifuatwa na Yehu. Yehu akawaamuru watu wake, “Muueni naye pia!” Nao wakampiga mshale akiwa garini kwenye njia ya kupanda Guri karibu na mji wa Ibleamu. Halafu alikimbilia Megido na kufia huko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ahazia, mfalme wa Wayuda, alipoviona akakimbia na kuishika njia ya Beti-Hagani (Nyumba ya Bustani), Yehu akamfuata mbiombio, akaagiza: Naye mpigeni katika gari lake! Wakampiga hapo pa kupandia Guri karibu ya Ibileamu; akakimbia hata Megido, ndiko alikokufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Ahazia mfalme wa Yuda alipoona hayo, akakimbia kwa njia ya nyumba ya bustanini. Yehu akamfuatia, akasema, Mpigeni huyu naye katika gari lake; wakampiga hapo penye kupandia Guri, karibu na Ibleamu. Akakimbilia Megido, akafa huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ahazia mufalme wa Yuda alipoona yaliyotukia alikimbia akielekea Nyumba ya Bustani, naye akifuatwa na Yehu. Yehu akawaamuru watu wake: “Mumwue naye vilevile!” Nao wakamupiga mushale akiwa ndani ya gari kwenye njia ya kupandia Guri karibu na muji wa Ibuleamu. Halafu alikimbilia Megido na kufia kule.