2 Kings 9:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kisha chukua chupa hii ya mafuta, ummiminie kichwani na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimekupaka mafuta kuwa mfalme wa Israeli.’ Kisha fungua mlango na kuondoka upesi utakavyoweza.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha chukua hii chupa na umimine mafuta juu ya kichwa chake, nawe utangaze, ‘Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Ninakupaka mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.’ Kisha ufungue mlango na ukimbie; usikawie!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, ukatwae ile chupa ya mafuta, ukayamimine juu ya kichwa chake, ukaseme, Bwana asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. Kisha ufungue mlango ukakimbie, wala usikawie.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kisha chukua chupa hii ya mafuta, ummiminie kichwani na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimekupaka mafuta kuwa mfalme wa Israeli.’ Kisha fungua mlango na kuondoka upesi utakavyoweza.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha chukua hii chupa na umimine mafuta juu ya kichwa chake nawe utangaze, ‘Hivi ndivyo asemavyo BWANA: Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.’ Kisha ufungue mlango na ukimbie; usikawie!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha chukua hii chupa na umimine mafuta juu ya kichwa chake, nawe utangaze, ‘Hivi ndivyo asemavyo bwana: Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.’ Kisha ufungue mlango na ukimbie; usikawie!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, ukatwae ile chupa ya mafuta, ukayamimine juu ya kichwa chake, ukaseme, BWANA asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. Kisha ufungue mlango ukakimbie, wala usikawie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kisha chukua chupa hii ya mafuta, ummiminie kichwani na kumwambia, ‘Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimekupaka mafuta kuwa mfalme wa Israeli.’ Kisha fungua mlango na kuondoka upesi utakavyoweza.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha kichukue hicho kichupa cha mafuta, uyamimine kichwani pake na kumwambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nimekupaka mafuta, uwe mfalme wa Waisiraeli. Kisha fungua mlango, ukimbie pasipo kukawia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, ukatwae ile chupa ya mafuta, ukayamimine juu ya kichwa chake, ukaseme, BWANA asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. Kisha ufungue mlango ukakimbie, wala usikawie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kisha utwae chupa hii ya mafuta, umumiminie juu ya kichwa na kumwambia: ‘Yawe anasema hivi: Ninakupakaa mafuta ukuwe mufalme wa Israeli.’ Kisha fungua mulango na kuondoka upesi utakavyoweza.”