2 Kings 9:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo wote wawili wakaingia chumba cha ndani na huko nabii akamtia Yehu mafuta kichwani na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema, ‘Nakupaka mafuta uwe mfalme juu ya watu wangu Israeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehu akainuka na kuingia ndani ya nyumba. Ndipo yule nabii akamimina mafuta juu ya kichwa cha Yehu, na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli: ‘Ninakupaka mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Mwenyezi Mungu, yaani Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa Bwana, yaani, juu ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo wote wawili wakaingia chumba cha ndani na huko nabii akamtia Yehu mafuta kichwani na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema, ‘Nakupaka mafuta uwe mfalme juu ya watu wangu Israeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehu akainuka na kuingia ndani ya nyumba. Ndipo yule nabii akamimina mafuta juu ya kichwa cha Yehu na kutangaza kwamba, “Hivi ndivyo asemavyo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehu akainuka na kuingia ndani ya nyumba. Ndipo yule nabii akamimina mafuta juu ya kichwa cha Yehu na kutangaza, “Hivi ndivyo asemavyo bwana, Mungu wa Israeli: ‘Ninakutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa bwana, yaani Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, yaani, juu ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo wote wawili wakaingia chumba cha ndani na huko nabii akamtia Yehu mafuta kichwani na kumwambia, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema, ‘Nakupaka mafuta uwe mfalme juu ya watu wangu Israeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipoondoka, akaingia nyumbani; humo akayamimina yale mafuta kichwani pake na kumwambia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Nimekupaka mafuta, uwe mfalme wao Waisiraeli walio ukoo wake Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, yaani, juu ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wote wawili wakaingia ndani ya chumba cha ndani na kule nabii akamutia Yehu mafuta juu ya kichwa na kumwambia: “Yawe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Ninakupakaa mafuta ukuwe mufalme juu ya watu wangu Israeli.