2 Peter 1:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Najua kwamba karibu nitauweka kando mwili huu wenye kufa, kama Bwana alivyoniambia waziwazi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sababu najua kwamba hivi karibuni nitaliweka kando, kama vile Bwana wetu Isa Al-Masihi alivyoliweka wazi kwangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninajua kuwa ni lazima nitauacha mwili huu kitambo kijacho kwani Bwana wetu Yesu Kristo amenionyesha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Najua kwamba karibu nitauweka kando mwili huu wenye kufa, kama Bwana alivyoniambia waziwazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Najua kwamba karibu nitauweka kando mwili huu wenye kufa, kama Bwana alivyoniambia waziwazi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu najua ya kwamba hivi karibuni nitaliweka kando, kama vile Bwana wetu Yesu Kristo alivyoliweka wazi kwangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sababu najua ya kwamba hivi karibuni nitaliweka kando, kama vile Bwana wetu Isa Al-Masihi alivyoliweka wazi kwangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionesha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Najua kwamba karibu nitauweka kando mwili huu wenye kufa, kama Bwana alivyoniambia waziwazi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani najua: siku iko karibu, nitakapolitoka hili hema langu, kama alivyonieleza Bwana wetu Yesu Kristo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana ninajua kwamba ninakaribia kuacha mwili huu unaokuwa wa kufa kama vile Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha waziwazi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha kwa wazi.