2 Peter 1:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama nuru inavyong’aa gizani, hadi kupambazuke na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hili linatufanya tuwe na ujasiri kwa yale waliyosema manabii. Na ni vizuri ninyi mkifuata yale waliyosema, ambayo ni kama mwanga unaoangaza mahali penye giza. Mna mwanga unaoangaza mpaka siku inapoanza na nyota ya asubuhi huleta mwanga mpya katika fahamu zenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka Siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inayong'aa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi itokee mioyoni mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyong’aa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo tunalishika neno la ufumbuo kwa nguvu sana, nanyi mnafanya vizuri sana mkiliangalia, maana ni mwanga wa kumulikia mahali penye giza, mpaka kutakapokucha, mpaka nyota iwakayo mapema iwatokee mioyoni mwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile tunaamini ujumbe uliotangazwa na manabii. Ninyi munafanya vema mukishikamana nao. Ujumbe huo ni kama taa inayoangaza pahali pa giza, mpaka wakati wa mapambazuko na wakati nyota ya asubui itakapoangazia mioyo yenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu.