2 Peter 1:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwamba hakuna mtu yeyote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jambo la muhimu kuliko yote ambalo ni lazima mlielewe ni hili ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko unaotokana na mawazo ya nabii.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwamba hakuna mtu yeyote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwamba hakuna mtu yeyote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Awali ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama alivyopenda nabii mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika Maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo, lakini, kumbukeni kwamba hakuna mtu yeyote awezaye kufafanua mwenyewe unabii ulio katika Maandiko Matakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo hili litambueni kwanza, ya kuwa hakuna neno la ufumbuo lililomo Maandikoni, linaloweza kufumbuliwa kimtu tu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbele ya yote, mujue kwamba hakuna mutu anayeweza kufasiria yeye mwenyewe unabii unaokuwa katika Maandiko Matakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mkijua neno hili ya kwamba hapana unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fullani tu.