2 Peter 1:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nabii hakusema kile alichotaka kusema. Lakini wanadamu waliongozwa na Roho Mtakatifu kusema ujumbe uliotoka kwa Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe wa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mwenyezi Mungu wakiongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hakuna ufumbuo wo wote ulioletwa kwa hayo, mtu ayatakayo; ila watu watakatifu wa Kimungu waliyasema yaleyale, waliyopewa na Roho takatifu.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana hakuna hata ujumbe wowote uliotetewa kwa mapenzi ya kimutu, lakini watu walipasha ujumbe wa Mungu wakiongozwa na Roho Mutakatifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.