2 Peter 1:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na kuishiriki hali yake ya kimungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani kupitia mambo haya, ili kupitia hayo mpate kuwa washiriki wa asili ya uungu, na kuokoka kutoka upotovu ulioko duniani unaosababishwa na tamaa mbaya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na kupitia haya, alitupa ahadi kuu mno. Ili kwamba kwa hizo mnaweza kushiriki katika kuwa kama Mungu na ukaepuka maangamizo ya kiroho yanayokuja kwa watu ulimwenguni kwa sababu ya mambo maovu wanayotaka.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na mpate kuishiriki hali yake ya kimungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na kuishiriki hali yake ya kimungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani kupitia mambo haya, ili kwa kupitia hayo mpate kuwa washiriki wa asili ya Kiungu na kuokoka kutoka katika upotovu ulioko duniani kwa sababu ya tamaa mbaya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hiyo, ametukirimia ahadi zake kuu na za thamani kupitia mambo haya, ili kupitia hayo mpate kuwa washiriki wa asili ya uungu, na kuokoka kutoka upotovu ulioko duniani unaosababishwa na tamaa mbaya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa namna hiyo ametujalia zawadi kuu na za thamani ambazo alituahidia, ili kwa zawadi hizo mpate kuziepa kabisa tamaa mbaya zilizomo duniani, na kuishiriki hali yake ya kimungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha tukagawiwa viagio vikubwa mno vya kutupa macheo kwamba: Kwa nguvu zao mtakuwa, kama Mungu alivyo, mkiyakimbia yanayowaozesha ulimwenguni, ndiyo tamaa za miili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kufuatana na hayo, ametupatia ahadi nzuri sana na kubwa mupate kuepuka uharibifu unaoletwa na tamaa mbaya za dunia na kushika hali yake ya kimungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.