2 Peter 2:1 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Bwana Mungu Mwenyezi wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hapo zamani walikuwepo manabii wa uongo miongoni mwa watu wa Mungu. Ndivyo itakavyokuwa miongoni mwenu hata sasa. Watakuwepo walimu wa uongo katika kundi lenu, watakaoingiza mawazo yao wenyewe yatakayowaangamiza watu. Na watafundisha kwa werevu ambao mtashindwa kujua kuwa ni waongo. Watakataa hata kumtii Bwana aliwanunua. Na hivyo watajiangamiza haraka wao wenyewe.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo walimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama vile watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu, ambao kwa siri, wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli hata kumkana Bwana wa pekee aliyewanunua na kujiletea juu yao maangamizi ya haraka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama vile watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Isa, Bwana wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kulitokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako walimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini kulikuwako hata wafumbuaji wa uwongo kwao wa ukoo wetu; vivyo hivyo hata kwenu wafunzi wa uwongo watakuwako, wataleta mafundisho wa kuangamiza watu, wamkane naye Bwana aliyewakomboa; hivyo watajiletea wenyewe mwangamizo utakaowafikia upesi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zamani manabii wa uongo walitokea kati ya watu, na ndivyo hivyo walimu wa uongo watakavyotokea kati yenu. Watu hawa wataingiza mafundisho mabaya sana ya uongo kwa siri, wakimukataa hata Bwana aliyewakomboa na kujiletea maangamizi upesi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia.