2 Peter 2:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni wakaidi na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kudharau mamlaka. Kwa ushupavu na kwa kiburi, watu hawa hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hukumu hiyo ni kwa wale ambao daima wanaofuata tamaa za udhaifu wao wa kibinadamu. Hiyo ni kwa ajili ya wale ambao wanadharau mamlaka ya Bwana. Walimu hawa wa uongo hufanya chochote wanachotaka, na hujivuna sana. Wala hawaogopi kuwanenea mabaya viumbe wenye nguvu walioko angani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni washupavu na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni wakaidi na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kudharau mamlaka. Kwa ushupavu na kwa kiburi watu hawa hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya mbinguni,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kudharau mamlaka. Kwa ushupavu na kwa kiburi, watu hawa hawaogopi kunena mabaya dhidi ya viumbe vya mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hasa wale wanaofuata tamaa mbaya za mwili na kupuuza mamlaka. Watu hao ni wakaidi na wenye majivuno, huvitukana na hawaviheshimu viumbe vitukufu vya juu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakaopata makali kupita wengine ndio wale wanaofuata miili migeni kwa kuwa na tamaa chafu; nao ndio wenye kubeza ukuu pasipo kuogopa, hujivuna wenyewe tu, nako kuwatukana wenye utukufu hakuwatetemeshi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na hasa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu. na kudharau mamlaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na zaidi atawaazibu wale wanaoishi kufuatana na tamaa mbaya za kimwili na kuzarau mamlaka ya Mungu. Walimu wale wa uongo ni wenye kiburi, wenye kujivuna, nao hawaogopi kutukana viumbe vitukufu vya mbinguni.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na khassa wale waufuatao mwili katika tamaa ya mambo machafu, na kudharau mamlaka. Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu;