2 Peter 2:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, hali wakifurahia njia zao za udanganyifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki karamu pamoja nanyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wamesababisha watu wengi kuteseka. Hivyo hata wao watateseka. Hayo ndiyo malipo yao kwa yale waliyofanya. Wanadhani ni jambo la kufurahisha kutenda dhambi ambapo kila mtu anaweza kuwaona. Wanazifikiria sherehe zenye matendo yasiyofaa hata wakati wa mchana kweupe. Hivyo wao ni kama madoa ya uchafu na ni fedheha mnapokula pamoja nao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, bali wakifurahia njia zao za udanganyifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, hali wakifurahia njia zao za udanganyifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki katika karamu zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki katika karamu zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, hali wakifurahia njia zao za udanganyifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kisha watalipizwa mapotovu yao. Hushangilia malafi na malevi ya kila siku, huwa kama madoa yachukizayo wakijiingiza kwa udanganyi wao hapo, mnapogawiana vyakula, tena napo hapo hula vibaya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakipatikana na madhara, ambayo ni ujira wa udhalimu wao, wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; wamekuwa ni mawaa na aibu wakifuata anasa zisizo kiasi katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watalipwa mateso kwa sababu ya mateso waliyoleta. Wanafurahia kutimiza waziwazi tamaa zao mbaya za kimwili muchana kati. Kufika kwao katika karamu zenu kunaleta haya na chukizo kubwa wanapofurahia mambo yao ya udanganyifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;