2 Peter 2:17 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji, na ukungu unaopeperushwa na tufani. Giza nene limewekwa tayari kwa ajili yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walimu hawa wa uongo ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayosukumwa na dhoruba. Mahali penye giza nene pameandaliwa kwa ajili yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji na ukungu upeperushwao na tufani, ambao giza nene limewekwa tayari kwa ajili yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji, na ukungu upeperushwao na tufani. Giza nene limewekwa tayari kwa ajili yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawa huwa kama visima visivyo na maji, tena kama mawingu yanayokimbizwa na ukali wa upepo; fungu lao, walilowekewa, ni lile giza jingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wale walimu wa uongo ni kama visima visivyokuwa na maji tena, wao ni kama mawingu yanayopeperushwa na upepo; makao yao yametayarishwa kwenye giza nzito.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hawa ni visiwa visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa: