2 Peter 2:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana wao hunena maneno matupu ya kiburi. Nao wanavutia tamaa mbaya za asili ya mwili, ili kuwashawishi watu ambao wanajiondoa kutoka kwa wale wanaoishi katika hatia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wanajisifu kwa maneno yasiyo na maana. Wanawaongoza watu katika mitego ya dhambi. Wanawatafuta watu ambao wamechana na maisha ya kutenda dhambi na wanawarudisha tena katika kutenda dhambi. Wanafanya hivi kwa kutumia mambo ya aibu ambayo watu wanataka kuyatenda katika mapungufu yao ya kibinadamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana wao hunena maneno makuu mno ya upumbavu na kwa tamaa mbaya za uasherati huwashawishi watu ambao ndipo tu wamejiondoa miongoni mwa wale wanaoishi katika ufisadi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana wao hunena maneno makuu mno ya kiburi cha bure, na kwa kuvutia tamaa mbaya za asili ya mwili, huwashawishi watu ambao ndipo tu wamejiondoa miongoni mwa wale wanaoishi katika ufisadi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Husema maneno makuu yasiyo na maana; hivyo, walivyozifuata tamaa za miili na kupitisha kiasi, huwaponza walioanza kuwakimbia wale wanaoendelea kujipoteza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wakinena maneno makuu mno ya kiburi, kwa tamaa za mwili na kwa ufisadi huwahadaa watu walioanza kuwakimbia wale wanaoenenda katika udanganyifu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana kwa masemi yao ya kujivuna na yasiyokuwa na maana, na kwa njia ya tamaa zao mbaya za kimwili, wanawavuta watu ambao wanaanza kuwaepuka, na wale wanaoishi katika udanganyifu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu: