2 Peter 2:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ipo methali isemayo: “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika matope!” Ndivyo ilivyo kwao sasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwao mithali zimetukia kuwa za kweli, zinaposema: “Mbwa huyarudia matapiko yake mwenyewe,” tena, “Nguruwe aliyeoshwa hurudi kugaagaa matopeni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walichofanya ni kama “Mbwa anayekula matapishi yake.” Na “Kama nguruwe aliyeoshwa, kisha anarudi kugaagaa matopeni.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ipo mithali isemayo: “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika matope!” Ndivyo ilivyo kwao sasa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ipo methali isemayo: “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika matope!” Ndivyo ilivyo kwao sasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli isemayo: “Mbwa ameyarudia matapishi yake mwenyewe,” tena nyingine yasema, “Nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli isemayo: “Mbwa huyarudia matapiko yake mwenyewe,” tena, “Nguruwe aliyeoshwa hurudi kugaagaa matopeni.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaagaa matopeni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ipo methali isemayo: “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine isemayo: “Nguruwe aliyekwisha oshwa hugaagaa tena katika matope!” Ndivyo ilivyo kwao sasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilikuwa kwao, kama fumbo la kweli linavyosema: Mbwa huyarudia matapiko yake, naye nguruwe aliyekoga hugaagaa tena matopeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kile kitu walichofanya kinaonyesha wazi mufano unaosema: “Imbwa amerudilia kula matapiko yake,” na: “Nguruwe aliyesafishwa amerudia tena kugaagaa katika matope!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini lile onyo la ile methali ya kweli limewapata: Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa kujifingirisha matopeni.