2 Peter 2:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yuko tayari, na Mwangamizi wao yuko macho!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao katika tamaa zao mbaya, walimu hawa watajipatia faida kwenu kwa hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, wala uangamivu wao haujalala usingizi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Manabii hawa wa uongo wanachotaka ni pesa zenu tu. Hivyo watawatumia ninyi kwa kuwaambia mambo yasiyo ya kweli. Lakini hukumu ya walimu hawa wa uongo imekwisha andaliwa kwa muda mrefu wala hawatakwepa. Mungu atawaangamiza, hajalala usingizi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yu tayari, na Mwangamizi wao yu macho!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yuko tayari, na Mwangamizi wao yuko macho!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao katika tamaa zao mbaya, watajipatia faida kwenu kwa maneno ya madanganyo waliyotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, ambayo haikawii wala uangamivu wao haujalala usingizi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao katika tamaa zao mbaya, walimu hawa watajipatia faida kwenu kwa hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, wala uangamivu wao haujalala usingizi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; wao ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala maangamizi yao hayasinzii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa tamaa yao mbaya watajipatia faida kwa kuwaambieni hadithi za uongo. Lakini kwa muda mrefu sasa Hakimu wao yuko tayari, na Mwangamizi wao yuko macho!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa choyo chao watawachuuza nanyi na kuwaambia maneno ya udanganyi. Lakini kuhukumiwa kwao hakukawilii tangu kale, nao mwangamizo wao hausinzii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa sababu ya tamaa yao mbaya ya mali, walimu hawa wa uongo watajipatia faida juu yenu kwa njia ya maneno ya uongo. Lakini tangia zamani hukumu yao imekwisha kutangazwa, nao hawatakawia kuangamizwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.