2 Peter 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(kwa sababu yale matendo mapotovu aliyoyaona na kuyasikia huyo mtu mwenye haki alipoishi miongoni mwao yalimhuzunisha siku baada ya siku):
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila siku mtu huyu mwema aliishi miongoni mwa watu walioharibika, na moyo wake mwema uliumia kutokana na uhalifu na uvunjaji wa sheria aliyouona na kusikia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(kwa sababu yale matendo mapotovu aliyoyaona na kuyasikia huyo mtu mwenye haki alipoishi miongoni mwao yalimhuzunisha siku baada ya siku),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(kwa sababu yale matendo mapotovu aliyoyaona na kuyasikia huyo mtu mwenye haki alipoishi miongoni mwao yalimhuzunisha siku baada ya siku):
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Loti aliishi miongoni mwa watu hao, na kwa siku nyingi moyo wake ulikuwa katika wasiwasi mkuu aliposikia matendo yao maovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani huyo mwongofu alikaa katikati yao, nayo matendo mapotovu, aliyoyaona, nayo aliyoyasikia siku kwa siku, yaliuumiza moyo wake mwongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana mutu yule mwenye haki aliishi kati ya watu wabaya, akiona na kusikia kila siku mambo yaliyochukiza roho yake ya haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
maaua mtu huyu mwenye haki akikaa kwao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sharia: