2 Peter 2:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ikiwa hivyo ndivyo, basi Mwenyezi Mungu anajua jinsi ya kuwaokoa wamchao Mungu kutoka majaribu, na kuwaweka waasi katika adhabu hadi siku ya hukumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Unaona namna ambavyo Mungu anajua kuwaokoa wale wanaomheshimu kutokana na matatizo yao. Na Bwana anajua jinsi ya kuwaweka watu waovu kifungoni hadi atakapowaadhibu siku ya hukumu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi Siku ile ya hukumu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ikiwa hivyo ndivyo, basi Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa wacha Mungu kutoka katika majaribu na kuwaweka waasi katika adhabu hadi siku ya hukumu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ikiwa hivyo ndivyo, basi Mwenyezi Mungu anajua jinsi ya kuwaokoa wamchao Mungu kutoka majaribu, na kuwaweka waasi katika adhabu hadi siku ya hukumu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, basi, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa katika majaribu watu wanaomcha Mungu, na jinsi ya kuwaweka waovu katika adhabu hadi siku ile ya hukumu,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana hujua kuwaokoa majaribuni wenye kumcha, lakini wapotovu huwaweka, wapatilizwe siku ya hukumu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, ni kusema kwamba Bwana anajua namna ya kuwaokoa wenye kumwogopa katika majaribu. Lakini anangojea kuwaazibu watu wabaya kwa Siku ile ya hukumu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;