2 Peter 3:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini siku ya Mwenyezi Mungu itakuja kama mwizi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; navyo vitu vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia na kila kitu kilicho ndani yake kitaunguzwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini siku atakayorudi Bwana itakuwa siku isiyotarajiwa na kila mtu kama ambavyo mwizi huja. Anga itatoweka kwa muungurumo wa sauti kuu. Kila kitu kilicho angani kitateketezwa kwa moto. Na dunia na kila kitu kilichofanyika ndani yake kitafunuliwa na kuhukumiwa na Mungu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu na vitu vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia na kila kitu kilichomo ndani yake kitaunguzwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini siku ya Bwana Mwenyezi itakuja kama mwizi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; navyo vitu vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia na kila kitu kilichomo ndani yake kitaunguzwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Siku hiyo, mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; vitu vyake vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia itatoweka pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi; ndipo, mbingu zitakapotoweka kwa shindo kuu, nayo yaliyoko tangu mwanzo yatayeyuka kwa kuchomwa na moto, hata nchi za kazi zilizomo zitateketezwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku Bwana atakaporudi, itatimia kama vile mwizi anavyokuja. Siku ile mbingu zitatoweka kwa shindo kubwa, na viumbe vyote vinavyoangaza katika mbingu vitayeyuka. Dunia na vitu vyote vinavyokuwa ndani yake vitateketezwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.