2 Peter 3:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mkiingojea siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi — siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu. Siku hiyo italeta mbingu kuchomwa moto na kutoweka, na vitu vya asili vitayeyuka kwa moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mnapaswa kuangalia mbele, kuiangalia siku ile ya Bwana, mkifanya kile mnachoweza ili ije mapema. Itakapofika, anga itateketezwa kwa moto na kila kitu kilicho angani kitayeyuka kwa joto.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
mkiingojea Siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi—Siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mkiingojea siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi — siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu, ambayo siku hiyo mbingu zitachomwa moto na kutoweka na vitu vya asili vitayeyuka kwa moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu. Siku hiyo italeta mbingu kuchomwa moto na kutoweka, na vitu vya asili vitayeyuka kwa moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mkiingojea hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mkiingojea siku ile ya Mungu na kuifanya ije upesi – siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kuharibiwa, na vitu vyake vya asili vitayeyushwa kwa joto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mwingoje siku ya Bwana, itakapokutia, mpate kumkimbilia, mbingu zitakapoyeyuka kwa kuunguzwa na moto, yaliyoko tangu mwanzo yatakapoteketea kwa kuchomwa na moto!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mukingojea na kuharikisha kuja kwa Siku ile ya Mungu; ndiyo siku mbingu zitakapoyeyushwa kwa moto, na viumbe vyote vinavyoangaza katika mbingu vitakapoyeyuka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
mkitazamia hatta ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka.